PHASE FAILURE RELAY

PHASE FAILURE RELAY  

Taarifa nzuri kwa mafundi na wateja  hasa wanaotumia  three phase katika kuendesha mitambo yao.  

Kuna mbinu ya asili yakutumia taa tatu mafundi wengi sana wanapenda kuitumia (red yellow  and blue ), kama ishara ya kujua kama umeme wote wa njia tatu unapatikana katika mfumo ,    Hivyo wakiona taa zote zinawaka wanakuwa na uhikaka , kuwa umeme uko sawa , hivyo huchukua kuwasha mitambo yao.  

Madhara ya njia  hii

  1.    Sio rahisi kugundua wakati gani tatizo limjitokeza , hasa kipindi mtambo unatemebea, ni rahisi sana kusitukia mitambo inaungua, au kubadili muzunguko  wakaati mwingine kuzima  

2.    Sio rahisi sana kujua umeme umeshuka kwa kiwango gani , hivyo hupelekea kuunguza mitambo yako , kwa sababu ya  undervoltage. China ya  380 v  ac  , kwa  30 % mpaka 40 %    

3.    Mifumo hii ni ngumu kujua wakati gani tatizo limeondoka , kwa sababu hakuna mifumo inayoonesha kuwa tatizo limeondoka, kwa maana ya kukosa kiashiria cha kidigitali  (ALARM )  

Sasa karibu uijue vizuri  (phase failure relay)

Phase failure relay ,  ni kifaa ya kielectronika ambacho kimetengenzwa kwa muunganiko wa koilli ya usumaku, au mikondo amuzi mbali mbali ya kidigitali, kwalengo la kiusalama Zaidi katika mifumo ya umeme , hasa katika umeme wa njia tatu, THREE PHASE SYSTEM

Lengo kuu la kutengenezwa kwa aina hii ya relay , ni kuleta suluhisho la matatizo yafuatayo

a.    Kushuka kwa umeme baina ya phase moja na nyingine

kikawaida kiwango kinachokubalika kati ya phase moja na nyingine huwa ni kati ya  380- 415 V, hivyo umeme ukishuka china ya  380 kwa asilimia 30-40% huleta madhara makubwa sana , ambayo hupelekea  kuungua kwa vifaa  au kushindwa kuendesha katika uwiano wa mwendo (speed staiki, )  

b.    Kupotea kwa phase moja

madhara makubwa ni kuungua kwa mitambo inayotumia phase tatu, au kuzima baadhi ya mifumo inayoendeshwa na phase husiku  

c.    Kubadilika kwa mzunguko wa phase,

hii hupelekea kubadili mwelekeo wa mzunguko moto , hivyo hupelekea kuleta madhara makubwa sana ikiwemo kuvunja vunja kila aina ya mifumo iliyotengenezwa kwa lengo la kukidhi mwendo wa moto.   Faida ya matumizi ya  pahse failure , kila changamoto itakapo jitokeza , kwa uharaka sana , kitazima mtambo na kutoa taarifa kwa mafundi kwa njia ya alarm, au kwa njia ya  simu , kutegemea ufungwaji wake na fundi husika ,

 

Service and sales Engineer  

Sensorite  Controls  limited  

maulizo yote , yawasilishwe kwa njia ya whats-app +255 714 025 426 / Au email : info@sensorite.co.tz