7- DAY PROGRAMED TIMER SWITCH

Habari za leo tena rafiki yangu

Ikiwa siku ya 05/100 ya kuandika makala ya ufundi .

Leo ninakuletea aina maalumu ya switch kwa matumizi maalumu inayoitwa 7 -DAY PROGRAM TIMER SWITCH

Kumpuni ya TRONIC, ANDELI na ABB , ni moja ya kampuni inayozalisha aina hii ya switch

UTENDAJI KAZI WA 7 -DAY PROGRAM TIMER SWITCH

Kama wewe ni fundi ama mtumiaji naamini utaelewa kwa maana Nimelenga Wewe

Vifaa vinavyolengwa kuwashwa na aina hii ya switch ni TAA, A/C , FRIDGE , MAGATE

Aina hii inatumia msingi wa muda halisia ambapo mtaalamu anaipa maelekezo ya KUZINGATIA Ili kuwashwa au kuzima vifaa vya umeme ndani ya wiki nzima kutegemea na uhitaji wa mteja.

mfano mteja anataka J3, saa 8:00 am , iwashe fridge na ikifika saa 9:00 pm izime , na siku ya J4 saa 6:00 am iwashe fridge na kuizima saa 14:00

Kwa upande wa taa pia inaweza kufanya vivyo kama nilivyoelekeza hapo,

KWA NINI AINA SWITCH HII NI MHIMU

  1. Kupunuza upotevu wa umeme pale mtu anaposahau kuzima taa am A/C
  2. Kukupa uwezo wa kuwasha na kuzimo mifumo yako hata kama haupo, mfano A/C inaweza kuwashwa na kukuta chumba cha baridi tayari kwa matumizi Hass kwa wanaofanya Biashara za ukumbi na Halls.
  3. Kupunguza uharibifu wa samaki na vitu vingine ambavyo hutegemea ubaridi , na makosa ya kusahau kuwasha ama kuchelewa kufika kazini

NB.

Utendaji huu wote unawezekana tu pale utakapo fanywa na fundi makini anayejua Utendaji kazi wa switch hii.

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOCHAGUA AINA HII YA SWITCH

  1. Nguvu endeshi (Power supply) hapa ni lazima ujue pale unapoenda kufunga panapatikana nguvu aina gani e.i 220VAC, 24V DC, 110VAc, hivyo ni wajibu wa fundi kufanya UCHAGUZI SAHIHI WA Ina ipi ya switchibitafaa
  2. Uwezo wa kuendesha mzigo (Current) hapa switch zinapishana Kuna 10A,16A,20A,25A, hivyo ni uamuzi wako kuchagua ipi itakufaa
  3. Idadi ya vitu unavyo taka kuendesha (Number of out put ) zipo timer switch zina output 1, 2, 3 au 4 , Ila pia idadi ya out put (matoleo) huendana na ongezeko la Bei.

Hapa ndipo mwisho wa ufafanuzi wetu, Karibu siku nyingine kwenye makala za ufundi.