PRESSURE TRANSMITTER

Habari za Asubuhi, rafiki yangu

Leo ikiwa siku 03/100, tunaenda kuangalia kifaa maalumu chenye uwezo wa kutafasiri Mgandamizo (pressure) kuwa taarifa za umeme (Electric signal )

Nini maana ya Pressure transmitter

Hiki ni kifaa kinachobadili taarifa za Mgandamizo halisi kuwa signali umeme Ili kuweza kueleweka na mfumo endishi (Control system) kama vile ECU , PLC , na vitu vingine vinavyofanana na hivyo. Kuwepo kwa pressure transmitter kunasaidia mfumo kuweza kuwasiliana na kufanya maamuzi sawa sawa na maelekezo (Program)

MATUMIZI YA PRESSURE TRANSMITTER

Kifaa kama hiki unaweza kukitumia kwenye Generator kwa kuangalia oil pressure, Boiler system, Viwanda vya uzalishaji , Air compressors n.k

MAMBO YA MSINGI KUZINGATIA UNAPOCHAGUA PRESSURE TRANSMITTER KWA MATUMIZI YAKO

  1. Process connection (Muungo)
  2. Media / malighafi (Upepo, Maji, e.t.c)
  3. Kiwango cha kupima (pressure range )
  4. Aina ya signali za umeme (0-20mA,. 4-20mA,. 0- 5mV, 0-10 V )

NB.

Ni muhimu Sana kusoma karatasi ya melekezo kabla ya kutumia ama kufunga kifaa hiki kwenye mtambo wako

Kwa ushauri na melekezo ya ziada usisite kuwasiliana nasi kwenye mawasiliano hapo chini.

Ahsante sana kwa muda wako,