SOLID STATE RELAY -SSR

Solid state contactor / relay

Na

Sensorite.co.tz

Karibu katika makala ya leo 16/06/2020

Tunaangazia katika technolojia mpya na kisasa katika namna nzuri na yenye utulivu wa hali ya juu.

Leo tumekuletea ufafanuzi juu ya Solid state relay, kama inavyoonekana hapo juu, huo ni mfano zipo za aina nyingi sana , kutegemea na matumizi.

Tuanze kwa kujua maaana yake halisi

Hizi ni aina za relay ambazo zinatumika kuwasha na kuzima , bila ya vitu kutembea Kama ilivyo kwenye kontakta zinazotumia usumaku na  springi.

Maana yake hakuna kitu kinachotembea kukifuata kingine, ( No moving parts while switching )

Muundi wa Solid state Relay

Kimsingi kabisa kabisa hizi relay zinatumia technolojia ya kielectronics , kwa njia ya mwanga, diode na infra-rays.  Na inakuwa na sehemu kuu mbili mhimu sana

  • Input signal ( siginali za kuwashia ), power supply

Hapa ndipo unaingia Umeme Mdogo Sana kwa ajiri ya kuwashia  3 – 32 V DC ,

  • (high voltage )Out put  terminal ( controlled load terminal )

Hapa ndipo tunafunga kifaa tunachotarajia kukiendesha, mara nyingi inakuwa AC ,. Msongo mkubwa Hadi  220 / 440 VAC 100A ,

Taahadhari ,

Ni mhimu Sana kusoma karatasi ya melekezo( data sheet ) kabla ya kulifunga ,ili kuepuka hasara ya kupigwa shorti na kuingiza relay

Lazima ujue kiwango Cha Umeme kinachoruhusiwa kuendesha na kuendesha

Ahsante Sana kwa kuendelea kufuatilia makala zetu.