NAMNA YA KUCHAGUA NA KUIFUNGA (PHASE FAILURE RELAY)

PHASE FAILURE WIRING / MATUMIZI

Kama tulivyo kwisha kugusia, phase failure relay inashughulikia Sana usalama wa mifumo ya njia tatu (three phase), na mambo ambayo inalenga Sana kudhibiti

  • Kupanda na kushuka kwa umeme (Under or over voltage)
  • Kubadilika kwa munguko ( phase sequence )
  • Kukatika / kupungua kwa fazi moja  (phase break / single phasing
  1. AINA ZA PHASE FAILURE

Phase failure relay, huwa zimegawanyika katika makundi tofauti kutegemea na kigezo cha Nguvu ya kuiendesha (Power supply ) na namna inavyowezwa kusimikwa kwenye paneli (Mounting )

Aina ya Power supply

  • Inayotumia umeme uleule unaoupima na kuudhibiti (Measuring voltage/ Dependent power supply  type )
  • Umeme wa pembeni (Independent power  supply )

Usimikwaji (Panel Mounting)

  • Rail mounting , pembe nne, insehemu kabisa ya moja kwa moja ya kupachika
  • 11 pole Plug , nyingi zinakuwa za duara
  • NAMNA YA KUIFUNGA KATIKA MFUMO

Kabla sijaelezea kwa undani, Naomba utambue kuwa hii tunayoungumzia  ni relay  , na sifa kuu ya relay yeyote ni kubeba umeme kidogo kwa muda mrefu. Hivyo ondoa fikira ya kuwa phase failure relay inabeba umeme wa mtambo mzima.

Hivyo phase failure pekee haitoshi kukamilisha lengo la udhibiti na ulinzi wa mfumo wako, badala yake ,  tunatakiwa kuwa na vitu vya ziada  ambavyo vinauwezo wa kubeba umeme mkubwa kwa usalama uanaostahili , unaweza ukawa na moja ya vifuatavyo

  • Motorized breaker / Breka inayotumia motor ili kuzima na kuwasha kadri itakvyohitajika
  • Contactor/ Kontactor , naamini unavielewa , vizuri
  • Solid state contactor / isiyotumia coil / usumaku

PHASE FAILURE INASEHEMU MHIMU NNE (4)

  • Power  supply/ Nguvu ya kuindesha

Hapa ndipo umeme kwa ajiri ya kuindesha relay Inafungwa, inaweza kuwa 24 V DC / 220/ 380V AC

  • Control terminal .

Hapa zinakuwa  aina mbili (Normally closed  NC  /  Normally Open  NO )Sehemu hii ndiyo inafungwa mfuatano na contactor unayoutumia kufanya maamuzi ya kuwasha au kuzima mtambo wako ( In series connection with power contactor )

  • Timer setting / sehemu ya kuseti muda

Eneo hili ni maalumu kwa ajiri ya kuambia relay itrip , kama tatizo litadumu kwa secunde kadhaa,  nihimu sana , ukikosea kidogo hapa ni rahisi sana kuunguza mtambo , ni mhimu sana kuzingatia mazingira ya changamoto kitaalamu , usibuni tu ili kurahisisha.

  • Indicating lights

Hizi mara nyingi ni taa , nyekundu na kijani , hii mara nyingi zinamsaidia fundi kuona kwa Mbali kama kuna shida au laa,  visual indicator (Green- Safe), Red – Power supply in on, Yellew – Trip , Pia  hizi zinabadilika kutegemeana na aina ya mzalishaji na matamuzi ya relay hiyo.

  • Monitoring terminal

Hapa ndipo sehemu unafunga phase zote zilizopo chini ya uangalizi, mara nyingi tunachukua kabla ya contactor kuu, kutegemeana na aina ya phase relay, zipo zinaruhusu phase zote na neutral na zingine phase zote.

Ahsante sana , kwa keendelea kufuatilia Makala zetu ,

Kwa maswali na maoni , wasili nasie

0734 277 385 | info@sensorite.co.tz