Instrument Transformers

Esitas | Current Transformers | Voltage Transformers | Epoxy Insulator
Instruments transformer

Habari rafiki na mufuatiliaji wa makala zetu za kiufundi ,

Kama mtaalamu katika tasnia ya umeme swala la usalama na swala la msingi sana , Leo tunakuletea makala fupi sana kuhusu INSTRUMENT TRANSFORMERS

INSTRUMENT TRANSFORMER NI NINI?

Instrument transformer- hiki ni kifaa cha kiulinzi au kiusalama, Kama lilivyojina lake, hizi ni aina za transformer ambazo hutumika katika kugeuza / kutafsiri dudusu (signal) za umeme mkubwa kwenda katia signal ndogo ambazo zinaweza kupimika kiurahisi kabisa,

Tunatambua kabisa vifaa vyote vya kiulinzi katika mifumo ya umeme hutumia umeme mdogo sana, hivyo kazi kubwa sana ya instrument transformer ni kugeuza mawimbi makubwa ya umeme kwenda katika hali inayoweza kupimika. mfano kwa PANELS METERS zote hutegemea signals kutoka kwenye kifaa hiki ili kuweza kupima voltage au power.

AINA ZA INSTRUMENTS TRANSFORMER

Kimsingi tunaweza kuwa na aina nyingi sana za instrument transformer kutegemea na matumizi,aina ya signals na mazingira zinapotumika

ili tusichanganyikiwe , basi tunaweza kuzigawa instrument transformer katika kipengele cha signals (Voltages or Current )

  1. Current instrument transformer – Hizi kushughulikia sana kugeuza current kubwa kuwa ndogo kiwango cha kupimika, unaweza kuwa HT,LV ,Indoor or outdoor kutegemea na matumizi na mazingira
  2. Voltage Instrument Transformer -Hizi pia hushughulikia na kugeuza voltage kubwa kwenda kwenye signal ndogo kabisa ambazo zinaweza kueleweka na panel meters na instrument mhimu za maamuzi (Controls instruments)

FAIDA ZA KUTUMIA INSTRUMENTS TRANSFORMERS

  1. Zinatuongezea usalama zaidi, badala ya kusafiri voltage 11KV kwenda control room tunatumia vifaa hivi na kupata 4 – 20 mA , signals ambazo PLC na systems zingine zinaweza kuelewa na kumudu bila shida yeyote
  2. Zinapunguza gharama ya miundombinu ya uandeshaji ,na usimamizi wa mitambo
  3. Ni rahisi sana kubadilisha pale zinapopat hitilafu ya kiufundi

BRANDS NZURI KAMA UNATAKA KUNUNUA INSTRUMENTS TRANSFORMERS

Instruments Transformers

Kwa leo naomba niishie hapo , natumaini umepata mwanga , kama unaswali lolote ,usisite kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano hayo juu, kwa njia ya simu ama email.