Habari rafiki,
Leo ikiwa siku ya 15/100 katika mfululizo wa makala za kiufundi , tutangazia SELONOID VALVE
Bila shaka unafahamu kuwa kwenye mtambo wowote katika tasnia ya uhandisi swala la kufunga na kufungua valve ili kuruhusu au kuzuia media fulani , ni swala amabalo halikwepeki ili kufikia mchakato wa uzalishaji
mfano,kwenye Generator Engine – katika tukio la kuwasha tunahitaji kufungua mafuta ili yaweze kuingia kwenye chumba cha muwako, pia tunaweza kufunga mtiririko wa mafuta ili kuzima engine.
Nini Maana ya Selonoid Valve ?
Selonoid Valve – Ni kifaa chenye matundu ya kuigizia na kutolea media kama (Upepo, kimiminika ) kinachoweza kudhibiti au kuruhusu kwa msingi wa kupandisha ama kushusha kizibo kwa kutumia athari ya usumaku unaozalishwa kwa umeme.
Hiki ni moja ya kifaa mhimu sana katika viwanda maana ni moja ya kifaa ambacho hufanya maamuzi ya mwisho baada ya kupokea maelekezo kutoka kwenye controller ,
Kusingekuwepo na technolojia hii basi kila mahali panapotakiwa kudhibiti au kurhusu palipaswa kuwepo na mtu jambo ambalo lingepelekea gharama ya uzalishaji kuwa juu, na vitu visinge nunulika.
Ni kweli tasnia ya automation imeondoa ajira nyingi sana lakini kwa kiasi kikubwa imeongeza usalama wa mafundi na mitambo kwa ujumla na kufanya upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa bei rahisi.
Utendaji Kazi wa selonoid valve
Kama nilivyotangulia kusema, Valve hizi hutumia misingi ya usumaku wa umeme ambapo uwepo kwa umeme usumaku huzalishwa na kusukuma ama kuvuta ili kutimiza dhima ya kufunga na kufungua , pale umeme unapoondoka ule usumaku hupotea hivi kile kizibo hurudi mahala pake kwa nguvu ya springi.
Aina za Selonoid Valve
Kwa kweli hapa usije ukakalili , aina zote hutegemea kigezo unachotumia mimi nitajaribu kutumia vigezo vifuatavyo
UMEME (COIL VOLTAGE)
- DC selonoid valve – Hizi aina hutumia umeme nyoofu (24V , 48 V 110 V DC) kufunga ama kufungua valve husika
- AC selonoid valve -Hizi hutumia umeme geu (AC 24V, 110V,220V 400V AC ) kufunga na kufngua
HALI YA KUFUNGA / WAZI
- Normal Open – Hizi ni selonoid valve ambazo muda wote zimefungua na zikipata umeme hufunga njia
- Normally Closed – Hizi ni aina ya selonoid valve ambazo muda wote zimefunga na zikipata umeme hufungua
IDADI YA MATUNDU (CONNECTION PORTS )
Hapa valve zinaweka kwenye mafungu mengi kwa kigezo cha ni matundu mangapi yanaruhusu hewa au kimiminika kuingia na mangapi yanaruhusu kutoa hewa nje ,mfano (5/3 3/2 1/2 6/3 )
MATUMIZI
- Pneumatic Solenoid valve – Hizi ni maalumu kwa ajiri ya kudhibit upepo
- Hydraulic Solenoid valve -Hizi ni maalumu kwa ajiri ya hydraulic fluid , hutmika sana kwenye mitambo ya ujenzi na hydraulic systems.
HITIMISHO
Kwa leo naomba niishie hapo kwa maoni na ushauri , usisite kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano yetu kwenye page ya Contacts.