Soft starter
habari rafiki yangu natumai umzima wa afya
leo ikiwa siku ya 08/100 za uandishi wa makala maalumu ya ufundi leo nimekuandikia kuhusu soft starter kwenye Ac induction motor
MSINGI WA DHANA YA SOFT STARTER
Kutokana na Sheria ya mwendo (law of motion) Kitu kilicho kwenye utulivu kinahitaji nguvu kubwa Sana kukianzishia mwendo na kinahitaji nguvu kidogo Sana kukifanya kiendelee kwenye mwendo wake.
Hivyo basi motor za umeme huhitaji nguvu kubwa kuianzisha ( transient current) Jambo ambalo hupelekea kuchemka kwa motor.
Soft Starter _ ni kifaa cha kieletroniki kinachofungwa kati ya chanzo cha umeme na motor Ili kudhibiti mtiririko wa umeme kwenda kwenye motor.
kifaa hiki pale unapowasha huanza kwa kuruhusu voltage kidogo kidogo Sana kwa muda Fulani mpaka motor inafikia katika speed yake ndipo hurusu umeme wote kutiririka kwenda motor,
FAIDA ZA SOFT STARTER
- Hudhibiti umeme mshituo (Transient Current)
Hupunguza kuchemka kwa motor (overheating)
- Huongeza uhai na Maisha ya motor
- Ni rahisi Sana kuwasiliana na PLC , control system
Kama umenunua Motor kwa thamani kubwa ni Bora ukiilinda motor yako kwa hakikisha unachagua Soft starter sahihi