Habari za leo msomaji wetu,
ikiwa leo siku ya 07/100 katika uandishi wa makala za kiufundi,
Kwanza naomba nikushukuru Sana kwa muda na utayari wako wa kufuatilia makala hizi.
Basi bila kupoteza muda wako leo nakuletea kifaa endeshi kinachojulikana kwa Variable Frequency Drive (VFD)
UTANGULIZI
Unapogusa VFD , utakuwa kwa namna moja ama nyingine umegusa “A/C motors” kwa VFD zimetengenezwa kwa ajiri ya kuendesha mota.
natumai umejifunza njia kadhaa za kuinzisha moto (method of starting motor). Direct on line , Star~ Delta ,VFD, soft starter, n.k, njia zote huzingatia Sana usalama wa motor yako, ndio maana uchaguzi wa njia sahihi unategemea Sana tarifa za motor na mzigo inayoendesha
JE NAWEZAJE KUBADILI MWENDO KASI WA MOTOR
Naamu , Ili Kuweze kubadilimwendo Kasi wa motor unapaswa kuathiri mambo mawili.
- Voltage – kwa kupunguza voltage utakuwa unapunguza mwendokasi (RPM) ya Moto mfano mzuri kwenye fani za majumbuni , Ile regulator hupunguza na kupandisha voltage
- Frequency (f) Kwa kupunguza ama kuongeza frequency utakuwa unaathiri mwendo kasi (rpm)
MAANA YA VARIABLE FREQUENCY DRIVE (VFD)
Variable Frequency Drive – ni kifaa cha kieletroniki kinachotumika kubadili frequency ya umeme kwenda kwenye motor Ili kupata mwendo stahiki. Kifaa hiki hutumika Sana pale panapokuwepo na uhitaji wa mwendekosi tofauti tofauti (RPM).
MUNDO NA UTENDAJI KAZI WA VFD
VFD Ili kuweza kutekeleza jukumu lake ,hapa chini ndio muundo
[AC] >>>>>>[RECTIFIER]>>>>>>>[CAPACITOR FILTER]>>>>>>>>[INVENTER]
[mchoro unakuja]
MATUMIZI YA VARIABLE FREQUENCY DRIVE
- Kuelekeza mtiririko wa Maji (Water pressure /flow control) hapa tuna kuwa na motor amabayo imefungwa pamoja na pump ,kadiri speed (rpm) inapopanda ndipo flow rate ndo inapanda .
NB.
faida moja kuu ya VFD ni kwamba imetengenezwa kuweza kuendeshwa na PLC aidha “Manual au automatic“
Uwe na siku njema , kwa ushauri na maoni usisite kuwasiliana nasi kwa email na Whatsapp +255(0)734 277 385