Ultrasonic Transmitter.

Ultrasonic level Sensor . 4-20 ma, RS 485 and Hart output
Level measurement using ultrasonic sensor.

Habari, ikiwa leo siku ya 55/100 katika uandishi wa makala za kiufundi kuhusu instrumentation.

Utrasonic level transmitter – Hiki ni kifaa cha utambuzi kinachozlisha sauti iliyo chini ya uwezo wa mwanadamu kusikia na kuituma pale sauti itakapokutana na kuzuizi chochote hurudisha mwangwi hivyo ili kutambua umbali gani ambapo hicho kizuizi kipo kutoka kwenye chanzo cha sauti hiyo.

Sauti ambayo mwanadamu anaweza kusikia ni chini ya (20,000 hertz or 20 kilohertz), zaidi ya hapo hawezi kusikia ,

UTENDAJI KAZI WAKE

Ultrasonic level transmitter – hufanya kazi katika misingi ya Mwendo(speed) wa ultrasound katika hewa (330m/s) na muda (t) iliyotumika kupata mwangwi ili kutambua umbali ambapo kuzuizi kipo , kitu chochote isipokuwa hewa kinawezwa kutambuliwa kizuizi.

Umbali (Distance ) D= Ultrasound speed x time

Demo 37: Display distance measured by ultrasonic sensor using module  7-segment-LED-N-Digits

KWANINI TUNALAZIMIKA KUTUMIA TEKNOLOJIA HII YA ULTRASONIC

Zifuatazo ni sababu za kiusalama zinazotulazimisha kutumia technoljia hii madhubuti,

  1. Upimaji wa chemikali hatarishi kwa mwanadamu, corrosive chemical.
  2. Kujali usafi wa mlaji hasa pale tunapokuwa na tunazalisha vyakula kwa ajiri ya matumizi ya binadamu, technolojia hii inapunguza uwezekano wa kugasa.
  3. Pale tunapopima viripuzi (flammable liquids ),kwa kutumia technoligia hii tunakwepa hatari ya kuzalisha moto kutokana na msuguano wa kiumeme
  4. Pale tunapoamua kupima mahali ambapo hatuwezi kupafikia kwa macho , hii hutumika sana kwenye vifaa tiba , (kujua uvimbe, mkao wa mtoto)

MAMBO YA MSINGI UNAPOHITAJI KUTUMIA AU KUNUNUA ULTRASONIC TRANSMITTER

1.Kwa sababu hizi sensor huzalisha current/ voltage maalumu kwa umbali fulani , basi ni muhimu sana kujua aina ya output unayotaka kupata, maana huwa hazitoi moja kwa moja umbali ,lazima uingize kwenye mfumo wa kutambua

2.Mazingira ya wapi unataka kuitumia hii transmitter ,ili kuapa kitu sahihi kwa matumizi sahihi

3.Mounting option , ni mhimu sana ujue unaenda kukifunga kwa namna ipi ,ili uweze kupata ukubwa sahihi

Nashukuru sana kwa kuweza kusoma makala hii mhimu, kama unachangaomoto yeyote ya kiufundi na sensor yeyote, usisite kuwasiliana nasi katika njia Contact