L E V E L M E A S U R E M E N T

U P I M A J I W A U S A W A

Habari rafiki ,

ikiwa leo siku ya 42/100 katika uandishi wa makala za ufundi katika tasnia ya instrumentation

Leo tunakuletea ufafanuzi juu ya utambuzi wa usawa / level katika mchakato wa uzalishaji (Industrial processing)

KWANINI TUNAHITAJI KUTAMBUA USAWA / LEVEL

Katika mchakato wa uzalishaji tunahitaji kutambua level ya malighafi au bidhaa kwa sababu zifuatazo

1.Kujua wakati gani itakupasa kuongeza malighafi , hivyo kuepuka hasara ya kupoteza muda pale malighafi zinapoisha ghafla bila taarifa (mfano unakuwa na mfumo wa maji, kwa kosa kifaa kinachotambua na kufuatilia level unijikuta ghafla maji yameisha hivyo kupelekea kusima kwa shughuli zote zinazotegemea maji )

2.Kupunguza athari za malighafi kumwagika kipindi unajaza (Over flow) fikiria kama unajaza mfuta kwenye tank kwa kutokujua unijikuta yamezidi ujazo na kumwagika hivyo ni rahisi sana kuleta upotevu na uchafuzi wa mazingira

3.Kurahisisha kufanya maamuzi ukiwa kwenye chumba chako cha kuendeshea – uwepo wa mifumo kama hii inakusaidia sana wewe mwendeshaji wa uzalishaji kufanya maamuzi au mtambo wako kufanya maamuzi kwa urahisi.

NJIA ZA UTAMBUZI WA USAWA *(LEVEL MONITORING )

1.Upimaji wa matukio (Point level measurement ) /Digital method- Hii ni njia inayotumika kupima level katika matukio maalumu JUU. CHINI (HIGH or LOW) Upimaji huu haushughuliki na level halisi ya malighafi husiku , mfano FLOAT SWITCH ni moja ya upimaji wa matukio , maji yakiisha inawasha pump na yakijaa inazima pump.

2.Upimaji mfuatano(Continuos level monitoring)/Analogoue method -Huu ni upimaji mhimu sana unakuwezesha wewe kama mtaalamu kuendelea kufuatili hatua kwa hatua toka chini mpaka juu , na hii ni moja ya njia mhimu sana katika usalama , hii inamsaidia mtaalamu kujua level muda wowote anapotaka.

MBINU ZINAZOTUMIKA KUPIMA WA LEVEL (LEVEL INSTRUMENTS )

1. F l o a t s w i t c h

2.Electromagnetic float switch

3.Utrasonic L e v e l transmitter

4.Magnetostrictive

5.P r e s u r e level transmitter

Usikose kwenye mwendelezo wa makala hii katika siku zijazo, waweza kusoma makala mbali mbali tulizoziandika kwa weledi mkubwa sana.

maoni na maswali wasiliana nasi kupitia namba hii +2 5 5 7 3 4 2 7 7 3 8 5 au email info@sensorite.co.tz