Habari za leo rafiki na mfuatiliaji wa makala kutoka sensorite.co.tz
Bila shaka unafahamu kuwa umeme husafari kutoka pointi moja hadi nyingine kupitia nyaya zilizovikwa Ngozi (Insulated cable’s) , kwa kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, Basi hufika mahali zinapaswa kufungwa kwenye mtambo au kituo cha maungo ( Terminal Block)
Cable terminal / lugs ni vipande vigumu vya copper au aluminum ambavyo hubanwa kwenye ncha ya waya Ili kurahisisha uungwaji kwenye mifumo ya umeme.
KWA NINI TUNAHITAJI CABLE TERMINAL & LUGS
Sababu kuu inayotusukuma kutumia cable lugs ni sababu za kiusalama , kwa kupunguza hatari ya kusababisha moto katika mifumo ya umeme pia kupunguza hatari ya kuunguza mitambo yetu kutokana na athari ya kulegeo kwa maungo (Loose connections ), hivyo basi tunashauriwa kuhakikisha maungo yote ya mwisho (Terminal connections ) yafanyike kwa kutumia cable lugs ,
ZIFUATAZO NI SABABU ZA MSINGI KWA NINI MATUMIZI YA CABLE LUGS NI SULUHISHO MADHUBUTI
1.Climping options (Uwezekano wa kubanwa) cable luga zote zinaruhusu kubanwa na kushikamana vizuri na waya kwa kutumia kifaa maalumu (CLIMPING TOOLS)
2. TIGHTING WITHSTANDING POWER (KUHIMILI MGANDAMIZO) Cable lugs zote zinahimili mgandamizo wa screw wakati wa kufunga kwa sababu ya ujazo na matilio yaliyotumika kutengeza kuliko fundo la waya wenyewe hivyo kupunguza hatari ya kukatika kipindi unakaza screw yako kwenye boksi la maungo (Terminal Box )
3.URAHISI WA KUBADILISHA – Matumizi mazuri ya cable lugs yankupa wewe fundi urahisi wa kubadilisha ,kufuatilia tatizo kwa urahisi pamoja na kuongeza nyaya kwa urahisi kuliko kutumia mafundo na misokoto ya nyaya hasa kwa upando wa controls system
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA UNAPONUNUA CABLE LUGS
- 1. UNENE WA WAYA (Cable size ) kabla hujaamua kununua cable lugs lazima ujue unene wa waya unaoenda kuufunga (10,25 35 50 70 120 mm2)
2. MUUNDO WAKE (CABLE LUGS TYPE) Sio kila lugs inafaa kutumika na matumizi yako, ni mhimu kujua aina gani ya lug itakufaa mfano (Pin type , Round type , Fork type n.k),kutegemea na matumizi yako ndio itakuwa msukumo sahihi wa kuchagua cable lug ipi ikufae
3.MATIRIO (LUGS MATERIAL) Kutegemea na aina ya waya wako na boksi la maungo ndivyo vitakazo amua kuchagua material sahihi ya cable lugs yako mafano (Copper, AL , Brass )
Kwa mahitaji ya kununua Cable lugs au Ushauri kuhusu cable lugs , usisite kuwasiliana nasi kupitia Contacts
Ahsante sana kwa muda wako , unaweza kusoma makala mbalimbali kwa kubonyeza NEXT au PREVIOUS