Habari rafiki,
Leo ikiwa siku ya 22/100 ya uandishi wa makala za kiufundi,
Leo nakuletea makala maalumu kuhusu (Emergency stop button)
Ukiwa kama mteja ni haki yako kuwa salama na ni jukumu la msingi Sana la fundi yeyote katika tasnia yake.
Kama tunavyofahamu asilimia kubwa ya mitambo hupambana kugeuza nisharti moja kwenda kuwa mwendo,
- Engine hugeuza nguvu ya mafuta kuwe mwendo
- Generator hugeuza mwendo wa Engine kuwa umeme
- Motor Hugeuza nguvu ya umeme kuwa mwendo
Katika mazingira hayo yote ni swala lisilopi gika kuwa kunaweza kutoka hitilifu ambayo inaweza kusababisha maafa au uharibifu wa mtambo wako ,hivyo katika mazingira kama tunahitaji kuzima mtambo kwa haraka Sana, hapo ndipo tunahitaji kuwa na Emergency stop button 🛑
MAANA HALISI
Emegency stop button 🛑 ni aina ya switch ambayo muda wote imefunga (NC) maalumu kwa ajiri ya kuzima mtambo wakati wa dharura.
VITU VYA KUZINGATIA KUHUSU EMERGENCY STOP PUSH BUTTON
- Raangi (Color Code ) Emergency switch lazima iwe rangi ya njano au Nyekundu
- Mounting ( Mahala pa kufungwa) Switch yeyote inayofungwa ni lazima ufungwe mahali panapo fikika Bila kuhitani kifaa chochote , nje ya panel , pia ndani ya panel kwa mazingira yatakapo tokea dharura unatokea fundi akiwa anafanya marekebisho .
- Contact (Normally Close) ni mhimu Sana Emergency stop button iwe NC , Ili itakapo sukumwa ifungue circuit.
- Label 🏷️ Ni Kitu cha msingi Emergency switch kuwekewa label Ili kurahisha utambuzi kipindi cha dharura
- Push and latch (Ya kunasa) Emergency switch lazima inase pale inaposukumwa Ili kurahisha na kuongeza usalama mpaka tatizo litakapo Isha .
Ahsante sana kwa kufuatilia makala zetu ,Karibu kwa makala zijazo na zilizopita