Habari rafiki yangu natumai umzima wa afya,
sisi team kutoka sensorite.co.tz hatujambo kabisa
leo ikiwa siku ya 11/100 katika uandishi wa makala maalumu ya ufundi leo nimekuletea kifaa maalumu kwa jina la kigeni la ACTUATOR
MAANA YA ACTUATORS
Actuator ni kifaa kinachozalisha nguvu halisia ya kuzunguka ama kupanda na kushuka Ili kuweza kuendesha Kitu kama vile valve ,gate na Jacks kutokana na nguvu ya umeme / hydraulic/ upepo
Actuator hutumika Sana kuendesha valve kwa kufunga na kufungua katika mifumo ya automation ,hivyo basi ni mhimu kujua kwa uchache kuhusu actuator ,
AINA ZA ACTUATORS
Actuators zimegawanywa kwa makundi mawaili Aina ya mwendo wake na kwa KUZINGATIA aina ya chanzo cha nguvu kama ni hydraulic,umeme ama upepo
AINA ZA ACTUATORS KWA KIGEZO CHA MWENDO WAKE
- Quoter Turn actuator Hizi ni aina za actuator ambazo huzalisha mzunguko wa robo duara (90 °) hivyo vitu vyote vinavyoruhusu kufunga na kufungua kwa mwendo wa robo duara.
- Multi-turn Actuator Hii ni aina ya catuator Ina ruhusu kutoa mizunguko mingi Ili kukamilisha zoezi la kufunga ama kufungua
- Linear Actuator Hii ni aina nyingine ya actuator ambayo hutoa mwenda wa kwenda mbele au nyuma katika mstari nyoofu (Linear motion)
MATUMIZI
Actuator hutumika Sana kwenye maeneo yote ya nayohusu kulinda mtiririko ( flow ) kwa kendesha Valve, gates na wakati mwingine hutumika kwenye magari kwa ya kufunga na kufungilia upepo
Makampuni makubwa Sana yanayojihusisha na utengenezaji wa actuator ni ROTORK, Flowserve, AUMA, BIFFI na mengine mengi Ila hayo ni machache
FAIDA YA ACTUATORS
- Huzalisha mwendo mdogo Sana ukilinganisha na motor za umeme
- Huzalisha nguvu kubwa Sana (Turning torque )
- Ni rahisi kutengeneza mawasiliano kutoka control room, (HARTZ, Profinet,Profibus n.k)
- Ufungwa wake ni rahisi Sana kwa sababu zimetengenezwa kwa ajiri ya valve na vitu kama tulivyojadili hapo juu.
Makala ijayo nitagusia kuhusu namna ya kuzifunga na kuzitumia
Ahsante kwa muda wako, kama unamaoni ushauri usisite kutuandikia katika barua pepe yetu ya info@sensorite.co.tz