POWER SUPPLY

Habari rafiki yangu,

Natumai u mzima wa afya,

leo ikiwa siku ya 10/100 katika uandishi wa makala za ufundi hasa kwenye eneo controls na instrumentation kama ilivyo dhima yetu.

Kwenye mitambo yote inayoendesha na umeme imegawanyika katika maeneo makuu mawili

Mfumo mkuu (Main power )na control system

Kwa upande wa controls system vitu kama (contactors, Relay,Timers,Switch , indicators ,PLC, I/O modules et.c),kwa ajiri kufanya maamuzi pamoja na usalama wa mitambo sawa sawa na maelekezo ya mtaalamu (Controls designers) kwenda kwenye motor ,Pump na Conveyors,

Mifumo hii huundwa na kufungwa ndani kabineti maarumu cha chuma / plastic kinachojulikana kwa jina Control panels

Moja ya Kitu cha msingi Sana kwenye control panels ni POWER SUPPLY,leo ndicho tutakiangazia

MAANA YA POWER SUPPLY

Hiki ni kifaa cha kieletroniki ambacho kimeundwa Ili kuzalisha umeme mdogo AC/DC kwa ajiri ya kuendesha controls system

AINA ZA POWER SUPPLY (TYPES)

  1. AC/DC converter Hii ni aina inayogeuza umeme geu kwa nyoofu (AC ~ DC ), 220/415VAC ~ to 110/48/24/12 /6 V DC
  2. DC / DC converter Hii hugeuza level ya umeme nyoofu katika uwiano tofauti au sawa kutegemea na matumizi 12V DC to 24VDC,. 24VDC to 24 VDC
  3. AC /AC converter Hii hugeuza kutoka umeme mdogo kwenda mkubwa au kinyume chake Ili kukidhi mahitaji ya controls systems (220VAC to 110VAC )

UMHIMU WA KUWA NA POWER SUPPLY

  1. Hurahisisha wakati wa kubaini tatizo
  2. Hupunguza hatari ya kuunguliwa na mfumo endeshi pale inapotokea voltage surge
  3. Hupunguza hatari ya kuunguliwa mfumo wako endeshi kwa sababu unatumia umeme mdogo na pia power supply zote zimetengenezwa kumeza miyumbo yote ya umeme(Voltage surge )
  4. Hurahisisha maboresho au nyogeza ya mifumo mingine (Control system expansion)

MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA UNAPOCHAGUA POWER SUPPLY

  1. Zingatia mahitaji ya mfumo wako (control system) kama 24V DC, 110VAC n.k
  2. Usalama / Protection Hapa hakikisha unachagua power supply amabayo inahimili power surges ,Ili kuepuka hasara ya kuunguliwa mifumo ya thamani kubwa
  3. Brand ,kwa maana ya mtengezaji , jiridhishe kuhusu ubora wa Brand husika , Lakini kwa uzoefu wangu Brand hizi zimekuwa zikafanya vizuri Sana katika eneo la Power supply. “Weidmuller, PHOENIX CONTACT, SIEMENS, ABB , Allen Bradley”, kwa kweli sijasikia Kesi kuhusu ubora
  4. Ufungwaji/Mounting ni mhimu Sana KUZINGATIA wapi itafungwa kwenye panel lako ,hivyo umbo na muonekano kwenye control panel lako ni mhimu. Ukizingatia kama fundi utakuwa umetimiza wajibu na usalama wa mitambo yako.

Kwa mahitaji ya Panel control power supply, usisite kuwasiliana nasi kwa email au WhatsApp

Ahsante uwe na siku njema ,