Habari za leo tena rafiki yangu natumai umzima wa afya
Ikiwa ni siku ya 06/100 katika uandishi wa makala za kiufundi leo na kuletea makala maalumu “I/O MODULES” kwenye matumizi ya computer elekezi za viwandani ama kwa jina maarufu ” Programmable Logic controller” PLC
UTANGULIZI
kama unavyofahamu mendeleo makubwa Sana ya technlojia yanavyozidi kuongezeka basi huna budi kupata hata sura kwa ufupi namna ambavyo wewe kama fundi ujuzi kidogo
Programmable Logic Controller (PLC ) hii ni aina ya computer ambayo inakubali kupokea maelekezo kwa kutumia lugha maalumu (programming language) Ili kuweza kutekeleza kazi maalumu Bila usimamazi wa mtu.
Programmable Logic Controller (PLC) – huwa haiwezi kabisa kuwasiliana na aina yeyote ya sensor (input sensor ) au indicator (output loads) kwa sababu ya aina ya signal. Kwani PLC huweza kuelewa taarifa zote katika mfumo lagha ya computer kwa maana 0/1.
Basi hapo ndipo Input and Out (I/O MODULES) husimama kati ya sensor zote zinatoa taarifa halisi kwenye mitambo iwe (Joto , pressure, Level ,limit Switch ) Ili kutafasiri kutoka kwenye lugha ya umeme (resistance, Voltage, Current)kwenda kwenye lugha ya komputa (0/1). Hili ndilo jukumu kuu Sana la hizo Module
AINA ZA I/O MODULES
- Digital Output/ input Modules Hii ni aina ambayo hutumika kutafasiri digital signal (tutajifunza baadae ) kwenda kwenye lugha ya computer
- Analogue Output/ Input module Hii hutafasiri Analogue signs kutoka ama kwenda kwenye mitambo kwenda kwenye lugha ya komputa
USHAURI
ukiwa kama fundi usikimbilie kubadilisha sensor au transmitter kwenye mfumo mpaka ujridhishe kuwa I/O module zinafanya kazi vizuri, Ili kuepuka lawama na kuingiza kampuni hasara .
Kumbuka dhumuni la kuajiriliwa mahali wewe kama fundi ni kupunguza break down na gharama za uanedeshaji, usikubali kuaibika unapokutana na Changamoto , tupigie ,tutakushauri
MWISHO
nakukushukuru Sana kwa muda wako ulioutenga kwa ajiri ya kujifunza nasi,.uwe na siku njema
HUDUMA ZETU
tunauwezo kukushauri na kukusaidia kugundua tatizo kwenye mifumo Bure(kwa njia ya simu ~ 0734 277 385 ) , kukuagizia spare yoyote inayohusa mambo ya automation (e.i. PLC , module na aiana zote za sensor)