Habari rafiki Karibu tena.
Ushawahi kujiuliza kwa nini lift tunazotumia kupanda na kushuka kwenye majengo makubwa huwa hazipitilizi floor uliyoielekeza.?
Basi ikiwa ni siku ya 04/100 za uandishi wa makala za kiufundi (Instrumentation Engineering), mahali ambapo mitambo inapewa uwezo wa kuamua kutegemea na mabadiliko ya mazingira na taarifa.
MAANA HALISI YA LIMIT SWITCH ?
Limit switch ni aina ya switch ambayo infanya maamuzi ya kuruhusu au kukata fununu (Signal) za umeme pale inaposogelewa na kitu Fulani lengwa. (Kwa maana rahisi kifaa hiki kinaruhusu au kukata mwendelezo wa sakiti ya umeme kutoka na maelekezo (Control programs)
Hivyo neno limit switch linazaliwa kwa kigezo kimoja tu kuwa kinafanikisha Kuzuia tu.
MATUMIZI YA LIMIT SWITCH
Limit switch hutumika kwenye mifumo yote inaendeshwa na umeme kama vile Milango , Gates,Conveyor belts, lift ,na vitu vingine vinavyohusika na kutembea kurudi.
Katika mazingira hayo tunahitaji limit switch Ili kulindi vitu kama hivyo visivuke mpaka vilivyowekewa na kuleta usalama kwenye mazingira yetu ya kazi na kuishi.
KARIBU TUANGALIE AINA ZA LIMIT SWITCH
Kwanza kabisa nikushukuru kwa muda kuendelea kijufunza na sensorite.co.tz
Aina zote za limit switch hutegemea aina na sifa ya utambuzi inayotumia Ili kufanya maamuzi kwenda kwenye mfumo enndeshi (Control system), kama nilivyojaribu kufafanusha hapo chini.
- Mechanical Limit switch– Hii hutegemea kuguswa kabisa na kitu husika ndipo ifanye maamuzi
- Proximity Limit switch – hii ni aina nyingine ambayo hufanya maamuzi pale tu kile kilichokusudiwa kinapo karibia mfaana inaweza mtu ,chuma , ama Kitu kingine kutegemea na matumizi
- Infrared limit switch. Hii ni aina ya limit switch inayotumia msinga wa mwanga (infrared rays )
- Magnetic limit switch. Hii haipishani Sana na proximity switch tofauti yake kuwa hii hutumia sifa ya usumaku kufanya maamuzi ,hivyo hapa huhusu Sana vitu vyenye asili ya chuma.
- zipo zingine aina japo hapo juu ndio maarufu
UCHAGUZI SAHIHI WA LIMIT SWITCH
Sio kila limit switch inafaa kwa matumizi yako,hivi ni mhimu KUZINGATIA mambo machache hapo chini.
- Aina ya umeme(signals)
- Aina ya controller inayohusika kufanya maamuzi
- mazingira (harsh, 🌧️, etc)
- Aina na material unayotaka Kuzuia
Kwa ushauri na ufafanuzi Zaidi usikose kuwasiliana na team ya ufundi kutoka au tembelea tovuti yetu (www.sensorite.co.tz)
Nakutakia majukumu mema , Kupata makala nyingine bonyeza Previous or Next