Habari za asubuhi rafiki yangu ,
leo tutaangazia kwa ufupi kuhusu kiongeza nguvu cha battery (battery charger ), hasa kwenye matumizi ya UPS na Generator ,
Maana ya Battery Charger
Hiki ni kifaa ambacho hutumika kuongeza nguvu kwenye battery , kwa lugha rahisi kucharge , lakini pamoja kuwa kinatumika kuliongezea nguvu battery , chenyewe pia huwa kinategemea nguvu kutoka kwenye chanzo kikubwa zaidi, kama vile Battery kubwa zaidi, (DC-DC charger ) au Umeme Geu (TANESCO) AC-DC charger , hivyo ni sheria ya asili kuwa mwenye nguvu ndiye anayemuongezea mwingine nguvu na kinyume chake .
Kwanini tunahitaji Battery Charger
kama tulivyosoma hapo juu, huwezi kuzungumzia kutunza nguvu za umeme bila kugusia Battery, Basi Battery pekee ndicho kifaa chenye uwezo wa kutunza nguvu ya umeme katika hali tuli (DC ), hivyo basi sababu kuwa ya kuhitaji battery charger ili tuweze kutunza nguvu ya umeme kwa matumizi ya dharura au baadae , mfano mzuri ni vile tunavyoweza kucharge simu zetu kisha zikijaa tunaondoka nazo , La sivyo ksingekwepo na technologia ya kutunza nguvu hiyo basi tungekuwa hatuweza kutembea na simu zetu kwa uhuru kama ilivyo leo
Aina za Battery Charger
Kutokana na matumizi kuna aina nyingi mno za charger , kwa leo tutaangazia aina moja wapo – TRICKLE CHARGER , bahati mbaya hakuna kiswahili chake ,
TRICKLE CHARGER
Hii ni aina ya charger ambayo hulisha msukumo(Voltage) na mgandamizo(Current ) kidogo sana kwa muda mrefu , ni moja ya charger hutumika kucharge na kulinda battery lisishuke nguvu yake kwa muda mrefu bila madhara , hi moja ya charger mhimu sana kwa matumizi ya kucharge battery la Generator , mara nyingi hutegemea nguvu kutoka TANESCO, ukikosea ukatmia battery charger tofauti na hii kwa ajiri ya kuwashia Generator yako, basi tegemea kuingia gharama ya kununu battery kila wakati .
Endelea kufuatilia makala zetu ,upate maarifa zaidi, na kama unahitaji ushauri usisite kutupigia , tutakushauri bure
.