Utungulizi
Habari za asubuhi ndugu yangu , kutokana na ukuaji kwa technolojia na kuongezeka kwa machaguo ,
Leo nakuletea utambulisho wa relay geu (Altenating relay )
Hii ni aina ya relay , ambayo inatumika kuwasha au kuendesha mifumo miwili au Zaidi, katika hali ya kupokezana .
Relay hizi zipo za kampuni mbali mbali kutokana na ubora na matumizi
Utendaji Kazi .
Kabla ya kutolea ufafanuzi , kwanza tuanze kwa kusoma mchoro ufuatao / kiambato hapa
Kwa kurejelea mchoro hapo basi , karibu upate maelekezo ya kina hapa chini
Neno “Altenalting ” geu ndilo linaleta taswira halisi ya utendaji wake , kwamba inageuka geuka
Pale switchi “ S1” itakapo washwa na relay kupata umeme muda huo huo itafunga kuwasha mzigo uliofungwa ( LOAD 1), na pale switch S1 itakapozimwa (LOAD 1 ) itazima , na endepo switch (S1) itakapo washwa kwa mara ya pili na relay kupata umeme kwa awamu hii relay itawasha mzigo no 2 (LOAD 2)
Hivyo tukio litajirudia mara kwa mara kwa mubadilishano LOAD 1 >>>>>LOAD 2 >>>>>>LOAD 1
MATUMIZI
- Kuwasha taa za rangi mbili tofauti katika chumba kimoja kwa kutumia switch moja
- Inatumika kwa kuendesho mifumi ya pampu za maji katika kujaza na kutoa maji kwenye tank la maji
- na mengine yatakayo fanana kutoka na ufahamu wako ,
nakushukuru sana kwa muda wako ,
na karibu ujifunze mambo mengi Zaidi kutoka kwenye team ya ufundi.