PHASE FAILURE WIRING / MATUMIZI
Kama tulivyo kwisha kugusia, phase failure relay inashughulikia Sana usalama wa mifumo ya njia tatu (three phase), na mambo ambayo inalenga Sana kudhibiti
- Kupanda na kushuka kwa umeme (Under or over voltage)
- Kubadilika kwa munguko ( phase sequence )
- Kukatika / kupungua kwa fazi moja (phase break / single phasing
- AINA ZA PHASE FAILURE
Phase failure relay, huwa zimegawanyika katika makundi tofauti kutegemea na kigezo cha Nguvu ya kuiendesha (Power supply ) na namna inavyowezwa kusimikwa kwenye paneli (Mounting )
Aina ya Power supply
- Inayotumia umeme uleule unaoupima na kuudhibiti (Measuring voltage/ Dependent power supply type )
- Umeme wa pembeni (Independent power supply )
Usimikwaji (Panel Mounting)
- Rail mounting , pembe nne, insehemu kabisa ya moja kwa moja ya kupachika
- 11 pole Plug , nyingi zinakuwa za duara
- NAMNA YA KUIFUNGA KATIKA MFUMO
Kabla sijaelezea kwa undani, Naomba utambue kuwa hii tunayoungumzia ni relay , na sifa kuu ya relay yeyote ni kubeba umeme kidogo kwa muda mrefu. Hivyo ondoa fikira ya kuwa phase failure relay inabeba umeme wa mtambo mzima.
Hivyo phase failure pekee haitoshi kukamilisha lengo la udhibiti na ulinzi wa mfumo wako, badala yake , tunatakiwa kuwa na vitu vya ziada ambavyo vinauwezo wa kubeba umeme mkubwa kwa usalama uanaostahili , unaweza ukawa na moja ya vifuatavyo
- Motorized breaker / Breka inayotumia motor ili kuzima na kuwasha kadri itakvyohitajika
- Contactor/ Kontactor , naamini unavielewa , vizuri
- Solid state contactor / isiyotumia coil / usumaku
PHASE FAILURE INASEHEMU MHIMU NNE (4)
- Power supply/ Nguvu ya kuindesha
Hapa ndipo umeme kwa ajiri ya kuindesha relay Inafungwa, inaweza kuwa 24 V DC / 220/ 380V AC
- Control terminal .
Hapa zinakuwa aina mbili (Normally closed NC / Normally Open NO )Sehemu hii ndiyo inafungwa mfuatano na contactor unayoutumia kufanya maamuzi ya kuwasha au kuzima mtambo wako ( In series connection with power contactor )
- Timer setting / sehemu ya kuseti muda
Eneo hili ni maalumu kwa ajiri ya kuambia relay itrip , kama tatizo litadumu kwa secunde kadhaa, nihimu sana , ukikosea kidogo hapa ni rahisi sana kuunguza mtambo , ni mhimu sana kuzingatia mazingira ya changamoto kitaalamu , usibuni tu ili kurahisisha.
- Indicating lights
Hizi mara nyingi ni taa , nyekundu na kijani , hii mara nyingi zinamsaidia fundi kuona kwa Mbali kama kuna shida au laa, visual indicator (Green- Safe), Red – Power supply in on, Yellew – Trip , Pia hizi zinabadilika kutegemeana na aina ya mzalishaji na matamuzi ya relay hiyo.
- Monitoring terminal
Hapa ndipo sehemu unafunga phase zote zilizopo chini ya uangalizi, mara nyingi tunachukua kabla ya contactor kuu, kutegemeana na aina ya phase relay, zipo zinaruhusu phase zote na neutral na zingine phase zote.
Ahsante sana , kwa keendelea kufuatilia Makala zetu ,
Kwa maswali na maoni , wasili nasie
0734 277 385 | info@sensorite.co.tz