Solid state contactor / relay
Na
Sensorite.co.tz
Karibu katika makala ya leo 16/06/2020
Tunaangazia katika technolojia mpya na kisasa katika namna nzuri na yenye utulivu wa hali ya juu.
Leo tumekuletea ufafanuzi juu ya Solid state relay, kama inavyoonekana hapo juu, huo ni mfano zipo za aina nyingi sana , kutegemea na matumizi.
Tuanze kwa kujua maaana yake halisi
Hizi ni aina za relay ambazo zinatumika kuwasha na kuzima , bila ya vitu kutembea Kama ilivyo kwenye kontakta zinazotumia usumaku na springi.
Maana yake hakuna kitu kinachotembea kukifuata kingine, ( No moving parts while switching )
Muundi wa Solid state Relay
Kimsingi kabisa kabisa hizi relay zinatumia technolojia ya kielectronics , kwa njia ya mwanga, diode na infra-rays. Na inakuwa na sehemu kuu mbili mhimu sana
- Input signal ( siginali za kuwashia ), power supply
Hapa ndipo unaingia Umeme Mdogo Sana kwa ajiri ya kuwashia 3 – 32 V DC ,
- (high voltage )Out put terminal ( controlled load terminal )
Hapa ndipo tunafunga kifaa tunachotarajia kukiendesha, mara nyingi inakuwa AC ,. Msongo mkubwa Hadi 220 / 440 VAC 100A ,
Taahadhari ,
Ni mhimu Sana kusoma karatasi ya melekezo( data sheet ) kabla ya kulifunga ,ili kuepuka hasara ya kupigwa shorti na kuingiza relay
Lazima ujue kiwango Cha Umeme kinachoruhusiwa kuendesha na kuendesha
Ahsante Sana kwa kuendelea kufuatilia makala zetu.